Anaandika Wakili Msomi Simon Patrick, aliyewahi kuwa Mwanasheria na Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga;
Nikilalamikia matokeo ya mechi nitakua nawakosea heshima Kagera Sugar kama moja ya timu bora kwenye ligi kuu sasahivi.
Najua itachukua zaidi ya miaka 100 Tanzania kupata technology ya VAR, lakini katika kipindi hiki Viongozi wetu wa mpira mmechukua hatua gani kuimarisha ligi yetu?
Katika kila mechi 10 utakuta 8 marefa wetu wameharibu mchezo kwa namna moja au nyingine, bahati mbaya zaidi sioni wakiendelea kuboresha viwango vyao.
Niwaombe bodi ya ligi kwenye adhabu mnazowapa vilabu kutokana na fujo za mashabiki, zingatieni kwa makini sababu zinazosababisha hizo fujo
Siimanishi natetea fujo za mashabiki ila nataka kuwajulisha kwamba kwa 99% zinasababishwa na waamuzi, hivyo tuwekeze sana kwenye capacity building ya waamuzi hii itainua mpira wetu wa Tanzania.
Mwisho nikiri timu yetu haikuwa na kiwango kizuri jana, ila nina imani na benchi la ifundi watalishughulikia.