Jana Yanga ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Bao la Carlos Carlinhos aliyefunga katika dakika ya 72 lilitosha kuihakikishia Yanga ushindi muhimu katika mchezo ambao Mtibwa Sugar walitumia takribani dakika 24 kupoteza muda
Yanga ikiwa na shauku ya kuondoka na alama zote tatu, Mtibwa Sugar wao walikuja na mpango wa kusaka alama moja, muda mwingi wachezaji wao waliutumia kuuguza majeraha ambayo mengi yalikuwa mbinu tu ya kupoteza muda na kupooza mchezo
Mwamuzi aliongeza dakika tano kufidia muda uliopotea. Hata hivyo wakati huo tayari Yanga ilikuwa imeshafunga bao lake
Β
ADVERTISE HERE