Kaze awashukia wachambuzi 'uswara'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Feb 2021
Kaze awashukia wachambuzi 'uswara'

Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema wiki hiii amejifunza utamaduni wa soka la Tanzania kutokana na kile alichokishuhudia wakati timu yake ikihaha kusaka matokeo

Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Mtiba Sugar uliopigwa dimba la Benjamin Mkapa jana na Yanga kuondoka na ushindi wa bao 1-0, Kaze amesema alishangazwa na mashambulizi na kejeli alizokuwa akizipata kutoka kwa wachambuzi wa soka nchini

"Kwa wiki moja hii nimejua tamaduni ya soka la Tanzania na nimejifunza mengi,Wachambuzi wa mpira wamekuwa wakinibeza lakini mimi niko poa. Ilikuwa ni kama mgonjwa amezidiwa kitandani halafu bado anapewa mzigo"

"Tulikuwa na wakati mgumu tukikosa ushindi katika mechi tatu zilizopita, tulifahamu mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar utakuwa mgumu, ulikuwa mpango wetu kutumia dakika za mwisho kusaka ushindi kwani tulifahamu wakati huo wachezaji wao watakuwa wameanza kuchoka"

"Ushindi huu umeturejeshea kujiamini na ari tuliyokuwa nayo, utatusaidia katika michezo inayofuata," alisema Kaze

Ilikuwa kama kampeni iliyoanza kushamiri baadhi ya wachambuzi wakimbeza Kaze baada ya timu kukosa ushindi katika mechi tatu mfululizo za ligi

Kama Yanga ingekosa ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar jana, katika baadhi ya redio mijadala ingekuwa mikali sana ilimradi tu kumuweka kwenye presha kocha na wachezaji wake

Hata hivyo Kaze ndiye kocha ambaye kikosi chake hakijapoteza mchezo msimu huu, wakicheza jumla ya mechi 33 za ligi kuu bila kupoteza

Hii ni rekodi ambayo Simba waliifikia msimu wa 2018/19 na sasa Yanga wanaweza kuivunja kama hawatapoteza mchezo utakaofuata ambao ni dhidi ya Coastal Union utakaopigwa March 04 jijini Tanga

Lakini ni nadra sana kuzisikia takwimu kama hizi zikizungumzwa na wachambuzi wa soka nchini pengine ndio maana huko mtaani kuna tetesi kuwa baadhi ya wachambuzi wanapewa 'mlungula' ili wasiandike wala kuzungumza mazuri ya Yanga lakini wayaanike zaidi mambo mabaya

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
7h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
11h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
12h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
12h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’