Kiungo na nahodha msaidizi wa Yanga Mukoko Tomombe amewashukuru mashabiki wa klabu hiyo kwa duwa na maombi yao kufuatia changamoto aliyopata katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar juzi
Wakati mchezo huo ukielekea ukingoni Mukoko alipata maumivu ambayo yalipelekea apewe huduma ya haraka uwanjani baada ya kuanguka na kupoteza fahamu
Nyota huyo raia wa DR Congo amesema sasa anaendelea vizuri na yuko imara kuendelea kuipigania Yanga
"Habari ya jioni (jana) wana yanga wenzangu, nashukuru sana kwa upendo wenu mlionionesha baada ya kuanguka uwanjani. Now naendelea vizuri Sana Mungu amesaidia tumepata point 3, mapambano yanaendelea Daima mbele Nyuma mwiko," ulisomeka ujumbe wa Mukoko alioweka kwenye ukurasa wake mtandao wa kijamii
Hii ni habari njema kwa mashabiki wa Yanga ambao wanafahamu umuhimu wa Mukoko katika kikosi cha timu yao
Jumapili ya wiki hii Yanga inakabiliwa na mchezo muhimu wa kombe la FA dhidi ya Kengold ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa