Kitaeleweka tu pale Kaunda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Dec 2017
Kitaeleweka tu pale Kaunda
Bado dhamira ya Yanga kuhakikisha inaanza kuutumia uwanja wake wa Kaunda kwa ajili ya mazoezi kuanzia mwakani iko palepale na zoezi la kujaza kifusi linaendelea licha ya changamoto ya mvua.

Aidha jana Katibu Mkuu wa Yanga charles Mkwasa alisema uungwaji mkono kutoka kwa wanachama na mashabiki wa Yanga umekuwa mkubwa ambapo michango kutoka makundi mbalimbali ya mitandao ya kijamii inaendelea kupokelewa.

Pia Mkwasa amewashukuru TANROADS kwa kusaidia kifusi cha kutosha kufanikisha ukarabati wa uwanja huku akibainisha kuwa Yanga inajipanga kukifikisha kifusi hicho Jangwani.

Aidha Mkwasa amedokeza kuwa alipata fursa ya kukutana na viongozi wanaosimamia eneo la Mto Msimbazi, waliosaidia kutanua mtaro ili kupunguza mafuriko Jangwani.

Mipango ya Yanga ni kuhakikisha uwanja huo unakuwa tayari kuanza kutumika kwa mazoezi ikiwezekana kuanzia mzunguuko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom.

Zoezi la maboresha ya uwanja huo litaendelea ambapo Yanga imekusudia kujenga uwanja wa kisasa utakaoweza kuchukua mashabiki 20,000.

Yanga itautumia uwanja huo kwa ajili ya mazoezi, michezo ya kirafiki na michezo yake ya ligi.

Mkwasa amesema wanakusudia kuufanya uwanja huo uwe moja ya chanzo kikubwa cha mapato ya klabu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’