Nchimbi afunguka uhaba wa mabao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Feb 2021
Nchimbi afunguka uhaba wa mabao

Mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi amesema hafurahii hali ya kutofunga mabao lakini jambo hilo halimsumbui hasa pale timu inapokuwa inafanya vizuri

Nchimbi aliyetua Yanga msimu uliopita akitokea klabu ya Azam Fc, wakati huo akicheza kwa mkopo Polisi Tanzania, amesema presha ya mashabiki haipaswi kumuondolea umakini katika kutimiza majukumu yake

"Timu hizi mbili (Yanga na Simba) zina presha sana, siku zote mashabiki wanataka ufanye vizuri tu. Wakati wote uwe tayari kutukanwa pale unapofanya vibaya lakini siku ukifanya vizuri watakusifu na kukupongeza"

"Muhimu ni kwa mchezaji kufahamu hali hiyo na kuweka juhudi kwa kile unachokifanya ili usitoke mchezoni"

"Nafahamu sijafunga muda mrefu lakini hilo halinisumbui kwani kitu muhimu kwangu ni kuisaidia timu iweze kupata matokeo. Kama nitafunga mimi ni vizuri lakini hata akifunga mwenzangu ni vizuri, jambo muhimu hapa ni timu kufanya vizuri," alisema Nchimbi

Nchimbi ana takribani mwaka mmoja hajafunga bao, ingawa katika kikosi cha Yanga amekuwa akitumika kimkakati zaidi

Katika msimu wake wa kwanza Yanga, Nchimbi alifunga mabao sita, msimu huu ametoa pasi mbili za mabao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’