Bado tunahitaji kuwa bora eneo la ushambuliaji - Kaze

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Feb 2021
Bado tunahitaji kuwa bora eneo la ushambuliaji - Kaze

Licha ya timu yake kuendelea kushikilia rekodi ya kutopoteza mechi katika za Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2020/21 unaoendelea, Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze, amesema bado ana kazi ya ziada ya kuimarisha safu yake ya ushambuliaji

Kocha huyo raiwa wa Burundi amesema anaendelea kufanyia kazi upungufu uliyomo katika safu hiyo kwa kuongeza utulivu na umakini wa kutumia vyema nafasi wanazozitengeneza za kufunga mabao.

Kaze alisema pia anahitaji kuona washambuliaji wake wanakuwa watulivu wanapokuwa jirani na lango la mpinzani ili kujihakikishia ushindi mnono na mapema.

Kocha huyo wa zamani timu za vijana za Fc Barcelona alisema wanahitaji kupata pointi tatu katika kila mechi ili kufikia malengo ambayo wanayatarajia na hatimaye kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na la mashindano ya Kombe ka FA.

"Hatuwezi kupata ushindi bila kufunga, tunatakiwa kuwa makini hasa katika nafasi tunazotengeneza kuhakikisha tunafunga mabao ili kuendelea kujiimarisha zaidi, kuendelea kubaki hapa juu tulipo, tunatakiwa kupambana na kila timu bila kujali nafasi na jina la mpinzani ambaye tunakutana naye," alisema Kaze.

"Tunahitaji kupambana kupata matokeo mazuri katika mechi zilizopo mbele yetu, sasa tunaenda kujiandaa kwa ajili ya mchezo wa FA dhidi ya Kengold, hakuna mechi rahisi na kwa sababu tunacheza mfumo wa mtoano, hatutawadharau," alisema Kaze.

Yanga itaikaribisha Kengold katika mechi ya mzunguko wa nne wa Kombe la FA itakayochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’