Mshauri Mkuu wa klabu ya Yanga Senzo Mazingisa amesema kukutana kwake na Kocha Mkuu wa Al Ahly, Pitso Masemane siku moja kabla ya mchezo kati ya Simba dhidi ya Al Ahly, hakukuwa na uhusiano wowote na mchezo huo
CEO huyo wa zamani wa klabu ya Simba, amesema Masemane ni mtu wake wa karibu na hivyo kuonana nae lilikuwa jambo la kawaida
"Ilikuwa ni lazima tuonane Jumatatu kwani tofauti na hivyo tusingeweza kuonana. Ni kitu gani ambacho naweza kumuambia Pitso ambacho hakifahamu kuhusu Simba?"
"Kwa kifupi nilikutana na rafiki yangu ambaye sijaonana naye muda mrefu..nilionana naye sehemu ya wazi ambayo kila mtu anaona na nilikunywa naye kikombe cha kahawa. Lakini naelewa niko kwenye ulimwengu wa Tanzania," alisema Senzo katika mahojiano ya eFM
ADVERTISE HERE