Kinadada wa Yanga Princess wanaendelea na msako wa ubingwa wa ligi kuu ya Wanawake jioni ya leo wakishuka dimbani kule mkoani Dodoma kuikabili Baobao Queens
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Disemba 2,2020 katika Uwanja wa Uhuru, Yanga Princess ilishinda magoli matano yaliyofungwa na Happiness Mwaipaja, Fatuma Makusanya, Emiliana Mdimu na mawili ya Aisha Masaka
Yanga Princess watakuwa na nafasi ya kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Wanawake hasa baada ya watani zao Simba Queens kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Ruvuma Queens
Yanga Princess wako kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa wamejikusanyia alama 34 wakifuatiwa na Simba Queens wenye alama 33 sawa na JKT Queens
Hata hivyo Yanga Princess wana mechi moja ya kiporo wanayocheza dhidi ya Baobab Queens huko Dodoma