Huu ndio mtego unaoikabili Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Mar 2021
Huu ndio mtego unaoikabili Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga Princess Edna Lema 'Morinho' amesema msimu huu Yanga imeingia katika mtego ambao kama hawatafanikiwa kuutegua, utawaumiza wachezaji na mashabiki wao

Lema ambaye kikosi chake cha Yanga Princess kinaongoza msimamo wa ligi kuu ya Wanawake wakiwa wamejikusanyia alama 38, amesema Yanga inakabiliwa na changamoto ya kujenga kikosi chake lakini wakati huohuo wanapaswa kutwaa ubingwa wa ligi kuu

"Kuna tofauti kati ya Yanga na simba. Yanga wameingia kwenye mtego wa kazi mbili kwa wakati mmoja. Kwanza kutengeneza timu yao na kuhakikisha wanapata matokeo mazuri na kutafuta ubingwa"

"Simba ni tofauti kwani wanaendelea kucheza kwenye kiwango chao ambacho wamekionesha katika misimu mitatu iliyopita baada ya kutengeneza timu yao"

"Yanga wataendelea kuwa kwenye presha kwa sababu wanahitaji ubingwa zaidi kuliko ambavyo wanafikiria. Mashabiki wanakiu ya kuona timu yao inarudi kwenye ubora iliokuwanao misimu mitano nyuma"

"Kwa sasa Simba wakikosa ubingwa halitakuwa jambo kubwa kwao tofauti na Yanga ambao kukosa ubingwa kunaweza kuwaathiri wachezaji na mashabiki wao," Lema aliiambia Clouds FM

Zaidi ya nusu ya wachezaji wa Yanga ni wapya, kuanzia duru ya pili ya msimu uliopita, GSM walijitosa kuisuka upya Yanga baada ya misimu mitatu ya kutofanya vizuri

Yanga imeanza vyema msimu huu ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi, lakini ikiwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
34m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
59m ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’