Katika mchezo wa ligi kuu kati ya Simba dhidi ya JKT Tanzania ambao ulipigwa juzi katika uwanja wa Benjamin Mkapa, kulikuwa na tukio la offside ya waziwazi ambalo Simba walifunaika nalo na kufunga moja ya mabao yake katika ushindi wa mabao 3-0

Tukio hilo limemuiba Msemaji na Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz ambaye amehoji hatma ya soka letu
"Maimamu wa Masjid Makandokando. Tutafika kweli kwa mtindo huu?," aliandika Nugaz katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Ikumbukwe ni hivi karibuni tu Yanga ililalamika kutotendewa haki na waamuzi katika baadhi ya mechi dhidi ya Mbeya City na Kagera Sugar ambapo katika michezo yote walinyimwa mikwaju ya penati ya dhahiri kabisa
Lakini hali ni tofauti kwa watani zao ambao wameendelea 'ku-enjoy' makosa ya waamuzi