Yanga imemaliza rekodi ya mwaka mzima kutopoteza mchezo kwenye ligi kuu ya Vodacom wakifungwa mabao 2-1 na Coastal Union
Ni matokeo ya kikatili sana hasa ukizingatiwa Yanga imeweka malengo makubwa ya kushinda ubingwa msimu huu
Bila ya kujali hilo, sisi mashabiki hatupaswi kuwalaumu sana wachezaji wetu kwani kupoteza mchezo leo, ni matokeo yaliyowaumiza sana
Kucheza mwaka mzima bila kupoteza mchezo katika ligi ni jambo la kishujaa, wachezaji wanastahili pongezi kwa kuipigania timu katika kipindi chote hicho
Hata kama Yanga isingefungwa leo, ingefungwa siku nyingine, ndivyo mpira ulivyo
Hauwezi kila siku ukawa wewe tu unayepata matokeo, ziko nyakati za aina hii ambazo zinaweza kuwa kipimo sahihi kwa sisi mashabiki juu ya upendo wetu kwa timu
Kama tulifurahi na wachezaji waliposhinda, basi tuhuzunike nao leo baada ya kufungwa
Sio wakati wa kutupiana lawama, benchi la ufundi, viongozi wameona kasoro zilipo bila shaka zitarekebishwa
Hata hao wanaoshangilia sana kufungwa kwa Yanga, wao msimu huu wamefungwa mara mbili..!