Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo kimeanza mazoezi kuelekea michezo ya kufuzu fainali za Afcon 2022 ikitarajiwa kucheza na Libya na Guinea ya Ikweta mwezi huu
Stars chini ya kocha Kim Poulsen wameanza mazoezi yao katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kabla ya mechi kuwania kufuzu Afcon, Stars itacheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Kenya, Harambee Stars
Nyota nane wa Yanga ni miongoni mwa wachezaji walioingia kambini katika kikosi cha Stars
Wachezaji hao ni Metacha Mnata, Yassin Mustafa, Bakari Nondo Mwamnyeto, Dickson Job, Deus Kaseke, Feisal Salum, Farid Mussa na Ditram Nchimbi
ADVERTISE HERE