Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dk Mshindo Msolla amesema mchakato wa kumpata kocha mpya umeanza ambapo Kamati ya Ufundi imepewa jukumu la kupitia CV za makocha walioomba kabla ya kumtangaza mshindi
Aidha wakati mchakato huo ukiendelea, aliyekuwa kocha msaidizi Juma Mwambusi amerejeshwa kuisimamia timu mpaka hapo atakapopatikana kocha mpya

Dk Msolla amesema wana imani na Mwambusi kwani alifanya kazi vizuri kabla ya kuugua na kuomba apumzike kwa muda ili atibiwe
"Tunategemea Mwalimu Mwambusi ataichukua timu wakati tunatafuta mwalimu mkuu, bahati nzuri yeye aliondoka vizuri, amepata matibabu klabu imemsaidia kwenye matibabu yake amepata nafuu.
"Hana ugeni wa timu tulikuwanae hadi kwenye Mapinduzi Cup kwa hiyo kurudi kwake sio jambo geni"
"Mwalimu mwingine tutaendelea na taratibu nyingine za kawaida, makocha watatuma CV zao zitakwenda kamati ya ufundi watazipitia na kuona yupi anafaa kwenye klabu yetu kwa sasa," amesema Dk Msolla