Baada ya kurejeshwa Yanga, Kaimu Kocha Mkuu Juma Mwambusi leo anaanza majukumu ya kukinoa kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria
Mwambusi ataiongoza Yanga kipindi chote ambacho uongozi utakuwa ukisaka kocha wa kudumu
Aidha kocha wa viungo Edem Mortotsi raia wa Ghana huenda nae akabaki kuendelea na majukumu yake
Yanga ina takribani wiki tatu za kujiandaa kabla ya mchezo wa kombe la FA dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa kati ya April 02/03 mkoani Rukwa
Mchezo wa ligi utapigwa April 07 dhidi ya KMC katika uwanja wa Benjamin Mkapa
ADVERTISE HERE