Kamati ya Utendaji Yanga yaridhia rasimu ya Mabadiliko

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Mar 2021
Kamati ya Utendaji Yanga yaridhia rasimu ya Mabadiliko

Kamati ya Utendaji ya Yanga imepokea na kuridhia rasimu za Mabadiliko ya Muundo wa Uendeshaji wa Klabu kutoka katika Kamati ya mabadiliko Katiba na kuruhusu mchakato kuendelea kwa hatua inayofuata.

Kikao cha Kamati ya Utendaji kilichokutana jana Makao Makuu ya Klabu Jangwani, chini ya Mwenyekiti wa Dkt. Mshindo Msolla, kilipokea rasimu hiyo baada ya mchanganuo mkubwa uliofanywa kutoka kwenye mapendekezo ya La Liga na Kamati Mabadiliko.

Kaimu Katibu Mkuu, CPA. Haji Mfikirwa amesema baada ya kupokea rasimu hiyo Kamati ya Utendaji ambayo ndio chombo cha juu cha maamuzi kwenye Utendaji wa Klabu imeridhia mchakato huo kwenda katika hatua ya kushirikisha wadau ambao ni hatua ya mwisho.

"Sasa tunakwenda katika hatua ya mwisho ambayo ni kuwashirikisha wadau kwa maana ya vyombo vya Serikali, kama BMT, FCC, Wizara na Wadau wa soka, kisha tutarudi kwa Wanachama na mwisho kabisa katika Mkutano Mkuu ambao ndio ngazi ya mwisho ya kutoa maamuzi kwa Klabu yetu kwa mujibu wa Katiba yetu ya sasa," amesema CPA. Mfikirwa

Amesema kwa sasa Kamati ya Mabadiliko ya Katiba itamalizia mapendekezo kadhaa ya Kamati ya Utendaji kisha kuanzia wiki ijayo mchakato usonge mbele.

"Kwenye muundo kuna mabadiliko kadhaa ambayo yamepitishwa, hivyo Kamati ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Wakili Raymond Wawa itakaa mapema wiki ijayo kuyaakisi mabadiliko hayo kwenye Katiba pendekezwa kisha tunatakwenda kuwashirikisha wadau wa Serikali," amesema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’