Msimu huu lugha ni moja tu Msimbazi, kurejesha taji la ligi kuu baada ya kulikosa kwa misimu mitano mfululizo.
Katika mkakati wa kuhakikisha mpango huo unafanikiwa, Rais wa Heshima wa Simba Bilionea Mohamed Dewji 'Mo' ameendelea kutoa hamasa ya kifedha kwa wachezaji ili kuhakikisha malengo yanafanikiwa.
Mo ameongeza bonas ya ushindi kwenye mechi za ligi kuu kutoka Tsh Milioni 20 hadi Tsh Milioni 40 kwa kila mechi isipokuwa mechi tatu kubwa dhidi ya Yanga, Azam Fc na Singida BS ambazo utaratibu wake wa bonas uko tofauti.
Aidha Mo ameendelea kutoa mamilioni kwenye michuano ya ligi ya mabingwa mpaka akiwa ametoa zaidi ya Tsh Milioni 500 kwenye hatua ya awali.
Utaratibu huo anatarajiwa kuendelea nao kuanzia hatua ya makundi pia.
ADVERTISE HERE