Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amemaliza mapumziko yake huko Brazil na anatarajiwa kurejea nchini wakati wowote kuendelea na majukumu yake ya kuinoa Simba
Robertinho alisafiri Brazil baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji Simba ikitoa taarifa kuwa kocha huyo anakwenda kushughulikia matatizo ya kifamilia na atarejea nchini leo
Simba inaendelea na mazoezi Mo Simba Arena chini ya kocha msaidizi Juma Mgunda wakijiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida BS ambao utapigwa Ijumaa
Robertinho alimuachia program za mazoezi Mgunda ambaye pia aliiongoza Simba kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Coastal Union Simba ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 na kutinga hatua ya 16 bora
Simba inakabiliwa na mechi muhimu mwezi Februari kwani baada ya mchezo dhidi ya Singida BS, watacheza mechi ya Kimataifa ya kirafiki dhidi ya Al Hilal kabla ya kusafiri Guinea kuikabili Horoya Ac kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Baadae Simba itarejea Tanzania kuikabili Raja Casablanca na kisha kufuatiwa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc kisha kusafiri nchini Uganda kuifuata Vipers Fc