Transfer

Tetesi za soka Ulaya, Jumatano Februari 1 2023

Joel JJ By Joel JJ
1 Feb 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumatano Februari 1 2023

Uhamisho wa mkopo kwenda Inter Milan haukuwa chaguo kwa beki wa England Harry Maguire, na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 atasalia Manchester United hadi angalau mwisho wa msimu. (Fabrizio Romano kupitia Twitter)

Manchester City wanapanga kumnunua mchezaji wa Leicester City James Maddison katika majira ya joto wakati mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 26 atakuwa amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa Foxes. (Mail)

Chelsea imeuliza Inter Milan kuhusu nia yao ya kumuuza kiungo wa kati wa Italia Nicolo Barella lakini klabu hiyo ya Serie A haikuwa tayari kumruhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kuondoka. (Tuttomercatoweb - kwa Kiitaliano)

Afisa MkuuMtendaji wa Inter Milan Giuseppe Marotta anasema ni chaguo la mlinzi wa Slovakia Milan Skriniar kutotia saini mkataba mpya na kuondoka bure wakati mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 27 utakapokamilika msimu wa joto. (Sport Mediaset, kupitia Football Italia)

Bournemouth ilikataa nafasi ya kumsajili kiungo wa kati wa Roma Nicolo Zaniolo baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia mwenye umri wa miaka 23 kubadili mtazamo wake kuhusu kujiunga na klabu hiyo ya pwani ya kusini. (Sky Sport Italia, kupitia Daily Echo)

Uhamisho uliomchukua kiungo wa kati wa Uhispania Isco, 30, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Sevilla mwezi Disemba, kwenda klabu ya Ujerumani Union Berlin uliporomoka. (Goal)

AC Milan wamekanusha kuwa kuna mvutano katika mazungumzo kuhusu kandarasi mpya na mshambuliaji wa Ureno Rafael Leao, 23, na mazungumzo yanafanyika "kwa njia ya kitaalamu". (Football Italia)

Barcelona ilijaribu kumsajili kiungo wa kati wa Morocco Sofyan Amrabat, 26, kutoka Fiorentina kwa mkopo ikiwa na jukumu la kununua lakini klabu hiyo ya Italia ilikataa ofa hiyo. (Sport - kwa Kihispania)

BBC

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
13h ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
14h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
16h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
16h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
17h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
17h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
17h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
18h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
18h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
20h ago
READ MORE →