Ruvu

Ruvu Shooting yahamia Morogoro

Joel JJ By Joel JJ
β€’
2 Feb 2023
Ruvu Shooting yahamia Morogoro

Baada ya kufanya vibaya katika mechi zake mbalimbali walizocheza kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kama uwanja wake wa nyumbani, Ruvu Shooting imetangaza kuhamia kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani, Morogoro

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, alisema mechi yao ya kwanza kutumia Uwanja wa Jamhuri itakuwa dhidi ya KMC FC ya Dar es Salaam ambayo itachezwa Jumapili.

"Tayari taratibu zote zimeshakamilika, Jumapili tutaanza kuutumia rasmi Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kama uwanja wetu wa nyumbani, nadhani baada ya hapo tutakuwa na mwendelezo mzuri kwa sababu kule ni kama nyumbani tu Pwani," alisema Bwire.

Hata hivyo, Bwire alikwepa kuhusisha uamuzi wa kuhama uwanja umetokana na matokeo mabaya waliyopata wakati wakicheza kwenye Uwanja wa Uhuru baada ya Uwanja wao wa Mabatini ulioko Mlandizi, Pwani kufungiwa.

"Uwanja hauchezi, unaocheza ni mpira, kama uwezo mdogo hata wakupeleke chumbani mwako watu watakufunga tu. Sisi tumejidhatiti kwenye uwezo na wala si kwa sababu tunapoteza sana Uhuru, ila Uwanja wa Jamhuri tuliuchagua tangu awali wakati uwanja wetu wa Mabatini Mlandizi ulipofungiwa," aliongeza ofisa huyo.

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
8h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
8h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
8h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
12h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
15h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
16h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
16h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
17h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
18h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
18h ago
READ MORE β†’