Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amesema amekiandaa kikosi chake kutandaza soka safi ya kushambulia katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida Big Stars ambao utapigwa kesho Ijumaa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Robertinho amesema itakuwa nafasi kwa wachezaji kuonyesha ubora wao mbele ya timu nzuri
"Lengo letu kama timu ni kushinda mchezo huu, nitatoa nafasi kwa wachezaji 11 bora, najua utakuwa mchezo mgumu lakini sisi tuna malengo yetu ambayo tunahitaji kuyatimiza"
"Nawaheshimu wapinzani lakini naiamini timu yangu, tumekuwa na mwendelezo mzuri na naamini kesho tutacheza vizuri na kuibuka na ushindi," alisema Robertinho
Robertinho amesema baada ya mazoezi ya mwisho leo atafahamu wachezaji 11 ambao atawatumia hapo lakini yeye anapendelea timu yake ishambulie kwa kasi na kuwa 'compact' katika eneo la kiungo