Transfer

Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi, Februari 02 2023

Joel JJ By Joel JJ
2 Feb 2023
Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi, Februari 02 2023

Everton wanataka kumsajili mshambuliaji wa Ghana Andre Ayew, ambaye anatarajiwa kuwasili Uingereza kwa mazungumzo, kwa uhamisho wa bure. Nottingham Forest pia inaweza kujaribu kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33. (Mail)

The Toffees pia wanaweza kutafuta kumsajili kiungo wa kati wa zamani wa Real Madrid na Uhispania Isco, 30, ambaye anapatikana kwa uhamisho wa bure. (Times - usajili unahitajika)

Everton ilishindwa kumnunua mshambuliaji wa Colombia Duvan Zapata mwenye umri wa miaka 31 baada ya ombi lao kukataliwa na Atalanta. (TeamTalk)

Hilo lilikuwa moja ya malengo 14 yaliyoripotiwa ambayo Everton ilishindwa kusaini siku ya mwisho. (Express)

Beki wa Chelsea na England Ben Chilwell, 26, ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na Manchester City msimu huu wa joto ikiwa mlinzi wa Ureno Joao Cancelo, 28, hatarejea kutoka kwa muda wake wa mkopo Bayern Munich. (Times - usajili unahitajika)

Wamiliki wa Chelsea hawatadai matokeo ya haraka kutoka kwa meneja Graham Potter kufuatia matumizi mabaya ya fedha ya mwezi Januari. (Guardian)

The Blues wanatazamiwa kuongeza usajili mwingine katika mshambuliaji Muingereza Jimmy-Jay Morgan, 17, ambaye atajiunga nao kutoka Southampton. (Sun)

Winga wa Chelsea kutoka Morocco Hakim Ziyech, 29, alituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa mmiliki wa klabu Todd Boehly alipokuwa akijaribu kukamilisha uhamisho wake wa mkopo kwenda Paris St-Germain. (Mirror)

Leeds United ilikataa nafasi ya kumsajili beki Mwingereza Axel Tuanzebe, 25, kwa mkopo kutoka Manchester United kabla ya dirisha la Januari kufungwa. (The Athletic, kupitia Metro)

Wakala wa mshambuliaji wa Liverpool na Brazil Roberto Firmino, 31, anaamini kuwa mazungumzo kuhusu kandarasi mpya katika klabu hiyo yatakamilika mwezi huu. (Sky Germany, kupitia Mirror)

BBC

More Stories

SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
15m ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
1h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
12h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
12h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
12h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
16h ago
READ MORE →
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
19h ago
READ MORE →
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
20h ago
READ MORE →
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
20h ago
READ MORE →
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
21h ago
READ MORE →