Mshambuliaji wa Brazil Gabriel Martinelli, 21, ametia saini mkataba mpya na Arsenal ambao utamweka katika klabu hiyo hadi msimu wa joto wa 2027. (Athletic - usajili unahitajika)
Newcastle United wameripotiwa kujiunga na mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham, 19, kutoka Borussia Dortmund msimu wa joto. (Football transfer)
Fiorentina waliachwa wakiwa wamechanganyikiwa na Todd Boehly huku mmiliki wa Chelsea akichukua jukumu la kujaribu kumsajili kiungo wa kati wa Morocco Sofyan Amrabat, 26, kwa mkopo siku ya mwisho ya uhamisho. (New York Times kupitia Talksport)
River Plate wanatazamiwa kupokea karibu euro milioni 32 swa na (pauni milioni 28) kufuatia kuhama kwa kiungo wa kati wa Argentina mwenye umri wa miaka 22 Enzo Fernandez kutoka Benfica kwenda Chelsea. (Fabrizio Romano kupitia Twitter)
Wakati huo huo, wachezaji wa nyumbani wa Chelsea wanahofia klabu italazimika kuwauza ili kuepuka matatizo ya usawa wa malipo (FFP) iwapo The Blues watakosa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu huu. (Telegraph - usajili unahitajika)
Tottenham walikuwa 'wamekaribia kukamilisha' uhamisho wa mshambuliaji wa Uhispania Gerard Deulofeu, 28, kabla ya mchezaji huyo wa Udinese kuondolewa uwanjani kwa msimu uliosalia mwezi Januari kutokana na jeraha la goti. (Fabrizio Romano kupitia Express)
Ajenti wa Moises Caicedo, 21, ameikosoa Brighton kwa kumnyima kiungo huyo wa Ecuador kuhamia Arsenal na kusema fursa hiyo "huenda isipatikane tena maishani". (Marca90 kupitia Ole - kwa Kihispania)
Winga wa Uingereza Jack Harrison, 26, anatarajiwa kusaini mkataba ulioboreshwa katika klabu ya Leeds United katika wiki zijazo. (Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Uhispania Isco, 30, bado anatafuta klabu mpya na amepewa ofa na timu kadhaa za Ligi ya Premia kwa mkataba wa muda mfupi. (90min)
BBC