Sean Dyche ameanza vyema majukumu yake ya kuinoa Everton baada ya leo kuiongoza timu hiyo kupata ushindi wa ba0o 1-0 dhidi ya vinara wa ligi Arsenal
Baada ya muda mrefu, hatimaye mashabiki wa Everton leo wamefurahia kandanda safi kutoka kwa timu yao na hivyo kufufua matumaini katika mkakati wao wa kusalia kwenye ligi kuu
Arsenal iliyokuwa imecheza mechi 13 mfululizo bila kupoteza kabla ya kipigo cha leo, walikuwa na wakati mgumu kukabiliana na vijana wa Dyche ambao walikimbia sana
Mlinzi wa kati James Tarkowski alifunga bao pekee la Everton kwenye mchezo huo akitumia vyema mpira wa kona uliochongwa na Dwight McNeil
Everton wameondoka kwenye eneo la kushuka daraja wakipanda mpaka nafasi ya 17 baada ya kufikisha alama 18
Licha ya kipigo Arsenal wanaendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama tano dhidi ya Manchester City
Alama 50 kwa Arsenal na alama 45 kwa Manc City huku timu zote zikiwa zimeshuka dimbani mara 20