Yanga imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo Fc
Dickson Job ndiye aliyeitanguliza Yanga kwa bao la kichwa kwenye dakika ya 43 akimaliza mpira wa kona kutoka kwa Stephane Aziz Ki
Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0. Kipindi cha pili Namungo walirejea wakiwa na kasi zaidi lakini kwenye dakika ya 51 Aziz Ki akafunga bao lake la tano msimu huu akitumia vyema makosa ya mlinda lango Deo Munish 'Dida'
Haikuwa bahati kwa Fiston Mayele kuongeza mabao yake kwani pamoja na jitihada zote hakufanikiwa kuweka mpira kambani
Kennedy Musonda nae alipata nafasi kadhaa lakini uimara wa Dida ulimfanya asifungue akaunti ya mabao kwenye ligi
Namungo walitengeneza nafasi kadhaa hasa kwenye kipindi cha pili lakini walikosa umakini mbele ya lango la Yanga hivyo kukosa nafasi nyingi
Wananchi wanaendelea kukaa kileleni kwa tofauti ya alama sita baad aya kufikisha alama 59


