Simba yalazimishwa sare na Al Hilal

Joel JJ By Joel JJ β€’ 5th February 2023


Simba yalazimishwa sare na Al Hilal

Mchezo wa Kimataifa wa kirafiki kati ya Simba dhidi ya Al Hilal umemalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1

Makapi Lilepo alifunga bao la Al Hilal kwenye dakika ya sita huku Simba ikisawazisha kupitia kwa Habibu Kiyombo kwenye dakika ya 81

Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira alifanya mabadiliko makubwa ya kikosi kwenye kipindi cha kwanza akiwapumzisha nyota wake muhimu

Lakini mabadiliko aliyofanya kwenye kipindi cha pili kwa kuwaingiza Mohammed Hussein, Shomari Kapombe, Clatous Chama, Pape Ousmane Sakho na Mzamiru Yasin yaliiongezea kasi Simba

Al Hilal walikuwa hatari zaidi kupitia mashambulizi ya kushitukiza kama sio uimara wa mlinda lango Beno Kakolanya, pengine wangefunga tena

Mchezo huu ulikuwa na umuhimu mkubwa kwa kila timu yakiwa ni maandalizi ya mwisho kuelekea hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa wiki ijayo

Simba itasafiri Guinea kuikabili Horoya Ac wakati Al Hilal wanakwenda Afrika Kusini kuumana na Mamelodi Sundowns


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.