Klabu ya Yanga imethibitisha kuwa winga Mghana Bernard Morrison atakuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili baada ya kupata majeraha ya nyama za paja
Daktari wa Yanga Moses Etutu amesema tayari Morrison alishaanza matibabu kama ilivyo kwa mlinda lango Aboutwalib Mshery ambaye anasumbuliwa na tatizo la goti
Mshery atakuwa nje kwa miezi minne ambapo anatarajiwa kusafiri Tunisia kwa ajili ya matibabu zaidi. pengine Wananchi watarajie kumuona tena uwanjani msimu ujao
Kwa Morrison ni kama Yanga ilicheza kamali kwani Mghana huyo ametumia muda mwingi nje ya uwanja kuliko ndani
Mara ya mwisho kwa Morrison kuonekana uwanjani ni Disemba 23 2022 katika mchezo wa ligi kuu ambao Yanga walishinda mabao 3-2 dhidi ya Azam Fc