Klabu ya Simba inatarajiwa kuzindua jezi maalum ambazo zitatumika kwenye hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Tukio la uzinduzi linatarajiwa kufanyika leo, Jumanne Februari 07 saa 1 usiku jijini Dar es salaam
Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limeigomea klabu ya Simba kutumia jezi aenye nembo ya wadhamini wao M-Bet kutokana na mgongano wa Udhamini ambapo Mdhamini Mkuu wa CAF kwenye michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho ni 1xBet
Simba huenda ikaendelea kutumia nembo ya VISIT TANZANIA badala ya M-Bet ili kukidhi matakwa ya CAF