Transfer

Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Februari 09

Joel JJ By Joel JJ
9 Feb 2023
Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Februari 09

Liverpool ni miongoni mwa vilabu vinavyovutiwa na mlinzi wa Everton Jarrad Branthwaite, 20, ambaye yuko kwa mkopo PSV Eindhoven. Manchester United na Roma pia wanamfuatilia beki huyo wa kati wa England chini ya miaka 20. (Mail)

Mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 33, yuko mbioni kuondoka Chelsea na kwenda Los Angeles FC.(Le10 Sport, via Metro).

Chelsea wapo kwenye mazungumzo ya mwisho mwisho na Thiago Silva kuhusu mkataba mpya wa mlinzi huyo wa Brazil utakaomvusha zaidi ya miaka 39 ya kuzaliwa kwake mwezi Septemba. (London Evening Standard)

Arsenal, Liverpool na Newcastle zote zinavutiwa na kiungo wa kati wa Ajax na Mexico Edson Alvarez, 25. (Caught Offside)

Arsenal pia wanaweza kuimgia katika mbio za kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Real Sociedad Mhispania Martin Zubimendi, 24, msimu huu kutokana na Barcelona kuelekeza nguvu zao za uhamisho kwingine. (Mirror)

Everton itafanya jaribio lingine la kumnunua mshambuliaji wa Ureno Beto, 25, kutoka Udinese ya Italia msimu wa joto baada ya kushindwa kufikia makubaliano mwezi Januari. (Mondo Udinese)

Leeds United imekataliwa na kocha wa Rayo Vallecano Mhispania Andoni Iraola, 40, kuchukua nafasi ya mkufunzi aliyetimuliwa Jesse Marsch huku timu hiyo ya Ligi kuu ikikabiliwa na hali ngumu zaidi katika kujaribu kumteua meneja mpya. (Onda Cero, via Express)

Tottenham inaweza kumsajili mlinda mlango wa zamani wa Manchester United na England Ben Foster, 39 kama mbadala wa Hugo Lloris, ambaye atakuwa nje kwa angalau wiki sita kutokana na jeraha la goti. Foster alitangaza kustaafu Septemba mwaka jana lakini anaweza kujiunga kwa mkopo wa muda mfupi. (Mirror)

Manchester United wametiwa moyo katika harakati zao za kumnunua kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 25, na mshambuliaji wa Uhispania Ansu Fati, 20, kutokana na La Liga kuwataka wababe hao wa Catalan kupunguza bili yao kubwa ya mishahara. (Mundo Deportivo, via Mail)

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Olivier Giroud anatarajiwa kujadili mkataba mpya na AC Milan. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, 36, alikuwa akisakwa na Everton mwezi Januari. (Fabrizio Romano) Mshambuliaji Joao Mendes, 17, mtoto wa gwiji wa Brazil Ronaldinho, anakaribia kujiunga na Barcelona baada ya kufuzu majaribio Nou Camp. (Star)

Kiungo nyota wa Kombe la Dunia wa Morocco Sofyan Amrabat, 26, alijitolea kucheza bila malipo ili kupata uhamisho wa kwenda Barcelona kutoka Fiorentina. (Mundo Deportivo, via Sun)

BBC

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
39m ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
1h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
3h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
3h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
4h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
4h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
5h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
5h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
5h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
7h ago
READ MORE →