Transfer

Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa Februari 10 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
10 Feb 2023
Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa Februari 10 2023

Manchester City wanataka ya kumsajili beki wa kushoto wa Chelsea na England Ben Chilwell, 26, katika dirisha la usajili la msimu wa joto. (CaughtOffside)

Chelsea wamemuweka mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 24, kama kipaumbele chao kikuu katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi. (90MIN)

Tottenham wanavutiwa na beki wa Crystal Palace Muingereza Marc Guehi, 22, wakati huu wakitaka kusajili mabeki wawili wapya wa kati kwa ajili ya msimu ujao. (Mail)

RB Leipzig huenda ikatafuta kumsajili tena kiungo wa kati Naby Keita, 27, msimu wa joto baada ya siku ya mwisho ya usajili wa Januari kukataliwa na Liverpool kumuachia mchezaji huyo wa kimataifa wa Guinea. (Bild)

Kiungo wa kati wa Barcelona na Ivory Coast Franck Kessie, 26, alikataa kuhamia Tottenham katika dirisha la uhamisho la Januari. (Sport)

Inter Milan wako tayari kufanya mazungumzo zaidi na Chelsea kuhusu mkataba wa kudumu wa kumnunua mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kwa sasa yuko kwa mkopo katika klabu hiyo ya Serie A. (Gazzetta dello Sport)

Ajax wanazidisha juhudi zao za kumpata mkurugenzi wa michezo wa Liverpool Julian Ward atakapoachana na majukumu yake Anfield mwishoni mwa msimu huu. (Telegraph)

Leeds wanafikiria kumnunua meneja wa Feyenoord Arne Slot ili kuwa meneja wao mpya. (Times)

Barcelona wanataka kuongeza mkataba wa nahodha wa klabu na kiungo wa zamani wa Uhispania Sergio Busquets, 34. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Liverpool wanamfuatilia kwa karibu nyota wa Birmingham City na timu ya taifa ya Uingereza ya vijana George Hall. Everton na Leeds pia wanavutiwa na kiungo huyo mwenye umri wa miaka 18. (Football Insider)

Barcelona itafuatilia mpango wa kumnunua beki wa kulia wa Bayern Munich na Ufaransa Benjamin Pavard, 26, katika majira ya msimu wa joto. (Mundo Deportivo)

Meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti huenda akachukua nafasi ya Tite kama kocha mkuu wa Brazil. (GeGlobo, via DefensaCentral)

BBC

More Stories

Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
1h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
5h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
5h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
6h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
7h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
7h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
8h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
9h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
22h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
22h ago
READ MORE β†’