Leo majira ya saa 1 usiku Simba itakamilisha maandalizi kuelekea mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Mchezo huo utafanyika katika uwanja wa Septemba 28, saa 1 usiku. Simba itafanya mazoezi ya mwisho katika uwanja huo
Habari njema kwa Simba ni kuwa mchezo huo utachezwa bila ya mashabiki na pengine ndio mchezo pekee ambao Horoya watacheza huko Guinea
Uwanja wa Septemba 28 umekosa sifa kulingana na vigezo vya CAF, Horoya wameruhusiwa kuutumia kwa mchezo dhidi ya Simba tu na katika nchi ya Guinea hakuna uwanja mwingine ulioidhinishwa na CAF
Horoya Ac watalazimika kwenda kucheza mechi zao ya nyumbani kwenye nchi jirani
Simba imekuwa gumzo katika Mji wa Konakr, mashabiki wengi wa soka nchini Guinea wanaifahamu Simba kutokana na mafanikio yake kwenye michuano ya ligi ya mabingwa
Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amesema wametua Guinea wakiwa na dhamira moja, kusaka ushindi na kama watakosa basi wataridhika kurudi na alama moja nyumbani
Simba iko kundi C pamoja na Horoya Ac, Raja Casablanca na Vipers
Raja Casablanca itachuana na Vipers Fc leo katika utakaopigwa saa 4 usiku