Klabu ya Azam Fc mwanzoni mwa wiki hii iliingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao utapigwa Februari 21 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Jana Azam Fc ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya KMKM na kuibuka na ushindi wa bao 1-0
Bao pekee la ushindi kwa Azam FC lilipachikwa kimiani na nyota wao Kipre Junior
Kaimu Kocha Mkuu wa Azam Fc Kally Ongala amesema baada ya kupoteza mchezo uliopita wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji, wanajipanga kushinda mchezo dhidi ya Simba ili kuwa na matumaini ya kumaliza katika nafasi tatu za juu
Azam Fc imelazimika kuisubiri Simba imalize mechi zake mbili za ligi ya mabingwa jana wakipoteza dhidi ya Horoya Ac kwa kufungwa bao 1-0
Mchezo wa pili watacheza Februari 18 dhidi ya Raja Casablanca katika uwanja wa Benjamin Mkapa