Klabu ya Liverpool huenda ikakubali kuwauza wachezaji wake nyota mwishoni mwa msimu ikiwemo mshambuliaji kinara kutoka Misri Mohamed Salah, 30. (Football Insider)]
Real Madrid wamefanya mawasiliano na kocha wa Liverpool Mjerumani Jurgen Klopp, 55, juu ya uwezekano wa kuchukua mikoba ya Mtaliano Carlo Ancelotti, 63, ya kuinoa miamba hiyo ya Uhispania kuanzia msimu ujao. (El Nacional - in Catalan)
Liverpool watakubali ofa ya wastani wa pauni milioni 15 ili kumuuza beki wa raia wa Cameroon, Joel Matip. (Football Insider)
Baadhi ya maafisa wa Chelsea wamechoshwa na hatua ya kiungo wao raia wa England Mason Mount, 24, kukataa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. (Telegraph)
Manchester United wapo katika mazungumzo na mshambuliaji wao kinara raia wa England Marcus Rashford, 25, ili aongeze mkataba. (GiveMeSport)
Newcastle wanasuka mpango wa kumsajili kiungo wa klabu ya Lazio na timu ya taifa ya Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 27, ambaye ana mkataba na klabu yake mpaka mwaka 2024. (Il Messagero, via Goal)
Manchester United wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Roma na raia wa Argentina Paulo Dybala, 29. (Calciomercato - in Italian)
Mshambuliaji wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ureno Joao Felix, 23, ambaye kwa sasa yupo Chelsea kwa mkopo, ndiye mchezaji kinara atakayewindwa na Real Madrid katika dirisha la usajili la mwishoni mwa msimu katika majira ya kiangazi.(Fichajes - in Spanish)
Paris St-Germain wanahaha kumnyakua kocha wa Manchester City Mhispania Pep Guardiola, 52. (El Nacional - in Catalan)
Nahodha na mshambuliaji kinara wa timu ya taifa ya England na klabu ya Tottenham Hotspur Harry Kane, 29, anatazamiwa kukataa ofa ya kujiunga na timu yoyote kubwa barani Ulaya ili kusalia katika Ligi ya Primia mwishoni mwa msimu huu. (Football Insider)
Kiungo wa klabu ya Barcelona na raia wa Ivory Coast Franck Kessie, 26, alikataa kujiunga na klabu ya Tottenham Hotspur katika dirisha dogo l usajili la mwezi Januari. (Sport - in Spanish)
Wapinzani wa jadi klabu za AC Milan na Inter Milan wote wanamtazamia kocha wa sasa wa klabu ya Lazio Maurizio Sarri, 64, kuwa kocha Mkuu wa klabu zao katika siku za usoni. (Il Messaggero, via Football Italia)
Nahodha na kiungo nyota wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard, 42, is "ana nia ya hali ya juu" ya kuchukua usukani wa kuinoa klabu ya Leeds ambayo hivi karibuni walimtimua kocha kutoka Marekani Jesse Marsch. (Football Insider)
BBC