Robertinho aipania Raja Casablanca

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 Feb 2023
Robertinho aipania Raja Casablanca

Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amewapongeza wachezaji wake kwa kuonyesha kiwango bora katika mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa dhidi ya Horoya Ac uliopigwa nchini Guinea jana

Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 katika mchezo ambao vijana wa Robertinho walipambana lakini wakakosa bahati ya kuweka mpira nyavuni

Robertinho amesema hawakuwa na mchezo mzuri sana kwenye kipindi cha kwanza lakini baada ya mapumziko walirudi uwanjani wakiwa bora zaidi na pengine hawakustahili matokeo waliyopata

"Kipindi cha kwanza wapinzani wetu walikuwa bora lakini sisi tulikuwa bora zaidi kwenye kipindi cha pili. Tumekosa nafasi mbili muhimu ndani ya eneo la hatari. Vijana wangu wamepambana, nawapongeza kwa jitihada zao, bahati haikuwa upande wetu leo"

"Huu ni mchezo wa ugenini ambao hautujaweza kufanikiwa sasa nasi tunarudi nyumbani kucheza mechi yetu ya kwanza. Malengo yetu ni kushinda mchezo huo"

"Najua tunakwenda kukabiliana na timu nzuri (Raja) lakini tutapata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wetu. Naamini wachezaji wangu watatumika vizuri ili kupata ushindi," alisema Robertinho

Mchezo dhidi ya Raja Casablanca utapigwa Jumamosi ijayo, Februari 18 saa 10 jioni

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
2h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
4h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
5h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
6h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
6h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
9h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
11h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
12h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
12h ago
READ MORE β†’