Transfer

Tetesi za soka Jumatatu, Februari 13 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
13 Feb 2023
Tetesi za soka Jumatatu, Februari 13 2023

Liverpool wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya Victor Osimhen kutoka Napoli. Mshambuliaji huyo wa Nigeria mwenye umri wa miaka 24 pia anasakwa na Manchester United. (Fichajes - kwa Kihispania)

Chelsea ni miongoni mwa vilabu vinavyomfuatilia mlinda mlango wa Brentford na Uhispania David Raya, 27. (Football.London)

Chelsea pia wanataka kumsajili winga wa Barcelona na Morocco Abde Ezzalzouli. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kwa sasa yuko kwa mkopo Osasuna. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Liverpool wanataka kumsajili mlinda mlango wa Anderlecht Mholanzi Bart Verbruggen kwa nia ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 kuwa mlinda mlango wao nambari moja. (Sun)

Mkufunzi mpya wa Everton Sean Dyche amepatia umuhimu mkubwa mlinda mpango wa mlango wa Uingereza Jordan Pickford, 28, kusaini mkataba mpya katika klabu hiyo. (Sun)

Kocha zamani wa Leeds Jesse Marsch huenda akaajiriwa Southampton baada ya kuondoka kwa Nathan Jones Jumapili, wiki moja baada ya kuondoka Elland Road. (Athletic- Usajili unahitajika)

Southampton pia wanavutiwa na kocha wa Torino Ivan Juric. (Mail)

Newcastle wako mbele ya Liverpool na Barcelona katika mbio za kuwania saini ya kiungo wa kati wa Eintracht Frankfurt na Japan Daichi Kamada, 26. (CaughtOffside).

Klabu za Southampton na Leeds zinamtaka kocha wa Argentina Marcelo Gallardo, 47, kuwa meneja wao mpya. (Football Insider)

Mshambuliaji wa Flamengo na Brazil Pedro, 25, yuko kwenye rada za West Ham. (Fichajes - kwa Kihispania)

Crystal Palace inamfuatilia mshambuliaji wa Celtic na Japan Kyogo Furuhashi, 28. (Football Insider)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
9h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
10h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
14h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
17h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
18h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
18h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
19h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
20h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
20h ago
READ MORE β†’