Huu unaweza kuwa msimu mzuri kwa Fc Barcelona kwenye ligi kuu ya Hispania, La Liga jana wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Villarreal
Bao la Pedri lilitosha kuipa Barca alama tatu muhimu ambazo zimewafanya waendelee kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi
Barcelona imefikisha alama 56 ikifungua tofauti ya alama 11 dhidi ya Real Madrid ambapo wana alama 45
Real Madrid wana mchezo wa kiporo kwani hawakucheza wikiendi hii kutokana na ushiriki wa michuano ya kombe la Dunia la klabu, wakitwaa ubingwa nchini Morocco
Barcelona chini ya Xavi Hernandez imekuwa bora, huenda msimu huu wakatwaa taji la La Liga
ADVERTISE HERE