Mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza zinazidi kupamba moto baada ya Manchester City kuichapa Aston Villa mabao 3-1 hapo jana na kupunguza gap la pointi dhidi ya vinara wa ligi hiyo Arsenal kuwa alama tatu
Mapema Manchester United ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Leeds United na kufikisha alama 46, wakiwa nafasi ya tatu tofauti ya alama mbili dhidi ya Man City na alama tano dhidi ya Arsenal yenye alama 51
Arsenal haikupata ushindi katika mechi mbili zilizopita wakifungwa na Everton bao 1-0 na juzi kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Brentford katika mchezo ambao pengine Arsenal hawakutendewa haki mwamuzi
Arsenal ina mechi moja pungufu ya Man City huku timu hizo zikitarajiwa kuchuana siku ya Jumatano katika mechi ya kwanza kwenye ligi msimu huu