Kikosi cha Simba kimerejea jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo wakitokea Guinea ambako walicheza mechi ya kwanza ya hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya Horoya Ac na kukubali kichapo cha bao 1-0
Jumamosi, Februari 18 Simba itakuwa dimba la Benjamin Mkapa kuikabili Raja Casablanca vinara wa kundi C ambao mechi yao ya kwanza walipata ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Vipers Fc

Watani zao Yanga nao watawasili baadae leo wakitokea Tunisia ambako walipoteza mechi ya Shirikisho dhidi ya US Monastir kwa kufungwa mabao 2-0
Yanga itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumapili kumenyana na TP Mazembe ambao ni vinara wa kundi D
Mazembe iliichapa Real Bamako mabao 3-1 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Lubumbashi, DR Congo
