Transfer

Tetesi za soka, Jumanne Februari 14 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
14 Feb 2023
Tetesi za soka, Jumanne Februari 14 2023

Atletico Madrid huenda ikakubali kumuuza mshambuliaji wa Ureno Joao Felix, 23, kwa Chelsea kwa euro 100m (£88.3m) msimu wa joto.

Klabu hiyo ya La Liga ilikuwa ikiomba kati ya euro 130m-140m (£115m-£124m). (Relevo - kwa Kihispania)

Kiungo wa kati wa Chelsea na Marekani Christian Pulisic huenda akaelekea kinyume na Felix, huku Atletico Madrid wakifikiria dau lililopunguzwa la mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye alisajiliwa na The Blues mwaka 2019 kwa pauni milioni 57.6. (Fichajes - kwa Kihispania)

Real Madrid inamfuatilia mshambuliaji wa Juventus Mserbia Dusan Vlahovic, 23, na nyota wa Tottenham wa Brazil wa Kombe la Dunia la Brazil Richarlison, 25, kama mbadala wa muda mrefu wa mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa Karim Benzema, 35. (ESPN)

Paris St-Germain huenda wakamweka mshambuliaji wa Brazil Neymar, 31 - ambaye walimsajili kwa kima cha yeuro 222m (£196m) kutoka Barcelona mnamo 2017 - kwenye orodha ya uhamisho wa majira ya joto. (Foot Mercato - kwa Kifaransa)

Mamlaka ya Uwekezaji ya Qatar itatoa ofa rasmi, la karibu pauni bilioni tano, kuinunua Manchester United yote ifikapo mwisho wa wiki. (Telegraph)

Bayern Munich wamejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Marcus Thuram, 25, kutoka Borussia Monchengladbach, lakini wapinzani wa jiji hilo Inter Milan na AC Milan bado wana hamu. (Sempre Inter)

Bayern Munich wameelekeza darubini yao kwa nahodha wa Tottenham Muingereza England Harry Kane, 29, huku Randal Kolo Muani, 24, owa Eintracht Frankfurt, akiorodheshwa kuwa mmbadala. (La Gazzetta dello Sport via Sempre Inter)

Mshambuliaji wa Athletico Paranaense Vitor Roque, 17, ambaye hivi karibuni alisaidia Brazil kushinda taji la Amerika kusini la wachezaji wa chini ya miaka 20, anaongoza orodha fupi ya uhamisho wa Arsenal majira ya kiangazi . (AS - kwa Kwa Kihispania)

Mshambuliaji wa Uhispania Sergi Roberto, 31, amekubali masharti ya kuongeza mkataba wake Barcelona ambayo yatamweka katika klabu hiyo hadi Juni 2024. (Fabrizio Romano).

49, Jesse Marsch - aliyetimuliwa na Leeds United wiki jana -kuchukua nafasi ya Nathan Jones wa Wales kama maneja wao. (TalkSport)

Kiungo wa kati wa Bayern Munich na Austria Marcel Sabitzer, 28, anasema "anajisikia vizuri" katika kipindi chake cha mkopo Manchester United na yuko tayari kufanya uhamisho huo kuwa wa kudumu. (Mail)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
4h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
4h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
4h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
8h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
11h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
12h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
12h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
13h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
14h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
15h ago
READ MORE β†’