Simba - Yanga - Azam

Spoti Arena kubwa kujengwa Dar

Joel JJ By Joel JJ
β€’
14 Feb 2023
Spoti Arena kubwa kujengwa Dar

Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, imepatiwa eneo la ekari 12 na Shirika la Nyumba (NHC) kwa ajili ya kujenga ukumbi wa Kimataifa wa kisasa wa Michezo (Sports Arena)

Akizungumza na wanahabari mara baada ya kukabidhiwa, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa leo Februai 14, 2023, amesema eneo hilo ambalo lipo Kawe, Dar es Salaam litakabidhiwa kwa mkandarasi na ujenzi utachukua muda wa miezi nane hadi kumi kukamilika.

Amesema ukumbi huo utakaokuwa na uwezo wa kubeba zaidi ya watu 16,000 unatarajiwa kuwa miongoni mwa Arena kubwa Afrika na kwamba kwa sasa Sports Arena kubwa ipo nchini Senegal, ambayo ina uwezo wa kubeba watu 15,000.

"Arena yetu itachukua watu 16,000 na tunategemea pia ichukue watu hadi 20,000 ili Watanzania wapate nafasi kushuhudia matamasha mengi katika ukumbi huo," alisema waziri.

Ameeleza kuwa dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha sekta ya burudani na michezo zinakuwa sekta zinazochangia kwa kiasi kikubwa kwenye pato la Taifa na wananchi wananufaika nazo

Habari Leo

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
37m ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
49m ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
1h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
4h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
8h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
9h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
10h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
11h ago
READ MORE β†’