Utayari wa Arsenal kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu, leo unapita kwenye jaribio la kwanza mbele ya mabingwa watetezi, Manchester City
Vinara hao wa ligi wanachuana na Man City katika mechi ambao hakuna mjadala wanahitaji kushinda ili kuwaaminisha mashabiki wao kuwa uwepo wao pale kileleni una sababu
Wanataka kumaliza ukame wa kukosa taji la ligi kuu kwa takribani miaka 19
Hii ni vita ya kuwania nafasi ya kwanza kwani kama Man City watashinda basi watawaondoa Arsenal katika nafasi hiyo licha ya kuwa washika bunduki wa London watakuwa na mechi moja ya kiporo
Huu ni mchezo wa kwanza kwenye ligi kati ya vilabu hivyo viwili msimu huu, ambao umecheleweshwa kutoka Oktoba 2022
The Gunners wameshuhudia uongozi wao kwenye kilele ukipunguzwa hadi pointi tatu, pointi zao zikishuka dhidi ya Everton na Brentford katika mechi za karibuni
Hata hivyo, bado watakuwa na mchezo mwingine dhidi ya City baada ya mechi ya leo usiku.
Kocha wa Gunners, Mikel Arteta anajua vyema hatari nyingi zinazoletwa na City baada ya kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu ya Uingereza pamoja na Pep Guardiola kama meneja msaidizi wa City kati ya 2016 na 2019.
Arteta najua anayo nafasi ya kushinda leo kwani mabingwa hao wa ligi wamekuwa na mwenendo mbaya ugenini katika mechi za karibuni wakipata vipigo mfululizo kwa Tottenham na Manchester United



