Simba

Simba yazindua kampeni ya ushindi Tegeta

Joel JJ By Joel JJ
β€’
15 Feb 2023
Simba yazindua kampeni ya ushindi Tegeta

Mwenyekiti wa klabu ya Simba Murtaza Mangungu amewataka mashabiki wa timu hiyo kuujaza uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Raja Casablanca ambao utapiwa Jumamosi, Februari 18

Akizungumza Tegeta leo katika tukio la uzinduzi wa hamasa kuelekea mchezo huo, Mangungu alisema hamasa ni kubwa kwa wachezaji na wameahidi watashinda mchezo huo wanachohitaji ni kuwaona mashabiki wao kwa wingi uwanjani

"Dhumuni letu (viongozi) tunataka uwanja ujae. Kwa namna tulivyozungumza na wachezaji na benchi ka ufundi wako tayari kutupa ushindi"

"Tunamshukuru Mhe. Rais kwa ahadi ya fedha. Nikiwa mwakilishi wenu napenda kuwambia wachezaji wamefurahi na tunamuahidi Mhe. Rais kuhakikisha tunashinda," alisema Mangungu

Nae Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema suala la ushindi kwenye mchezo dhidi ya Raja Casablanca sio mjadala lakini muhimu ni mashabiki kujitokeza kwa wingi kujaza uwanja wa Mkapa ili kuwapa hamasa wachezaji

"Tunataka Jumamosi tushinde, lakini ili kufanikisha jambo letu kwa urahisi tunatakiwa tuujaze uwanja. Tunakwenda kuwalipia kisasi ndugu zetu waliokula bao 6, kama Taifa hatuwezi kukubali jambo hilo liendelee. Tunakwenda kuwaonyesha sisi sio vilaza, sisi ni Simba Sports Club"

"Hii ni mechi ya kihistoria, tukijaa mashabiki 60,000 hakuna namna ya Raja AC kutoka," alisema Ahmed

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
7h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
8h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
8h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
12h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
15h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
16h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
16h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
17h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
18h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
18h ago
READ MORE β†’