Kiungo mshambuliaji Feisal Salum ambaye yupo kwenye mgogoro na klabu yake ya Yanga, amenusurika katika ajali ya gari iliyotokea mchana wa leo Jumatano, Fuoni Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.
Ajali hiyo imehusisha gari yake aina ya Harrier nyeupe yenye namba za usajili Z 160 MW dereva akiendesha mwenyewe alikuwa akitokea Fuoni kituo cha zamani akielekea Mjini
Gari yake ikagongana na Bodaboda yenye namba za usajili Z 423 KL. Katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza madhara makubwa zaidi ya gari kuharibika mbele na Bodaboda imeharibika
Mkuu wa kituo cha Polisi Fuoni amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo
"Ni kweli imetoka ajali hapa Fuoni Gari aina ya Harrier imegongana na Bodaboda, Gari ni ya yule bwana mdogo mchezaji wa Yanga Fei, lakini ni ajali ndogo tu hakuna aloumia". Mkuu wa Kituo Cha Polisi Fuoni alibainisha



