Yanga

Kamwe amtetea beki mpya Yanga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 Feb 2023
Kamwe amtetea beki mpya Yanga

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amewatoa hofu wapenzi na wanachama wa klabu hiyo kuwa ni suala la muda tu watamuona beki wao mpya Mamadou Doumbia

Tangu alipotua Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo, Doumbia aliitumikia Yanga kwa takribani dakika 30 kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Rhino Rangers

Kamwe amesema Doumbia anaendelea kuzoeana na wenzake katika viwanja vya mazoezi na Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema nyota huyo yuko tayari

"Kocha Nabi ameridhishwa na maendeleo yake mazoezini, nafikiri ni suala la muda tu mashabiki watamuona uwanjani. Doumbia ni beki mzuri sana Mwalimu alihakikisha anamuandaa vizuri kuepuka kuathiri muunganiko ambao tayari ametengeneza pale kwenye safu ya ulinzi," alisema Kamwe

Baada ya kuruhusu mabao mawili ya aina moja kwenye mchezo dhidi ya US Monastir, kumekuwa na midajala miongoni mwa mashabiki wa Yanga huku wengine wakihoji kwa nini Doumbia hatumiki

Beki huyo mrefu alikuwa nahodha wa kikosi cha timu ya Taifa ya Mali kilichoshiriki michuano ya CHAN huko Algeria

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
1h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
1h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
2h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
5h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
9h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
10h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
11h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
12h ago
READ MORE β†’