Babake mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi alifanya mazungumzo na PSG siku ya Alhamisi huku wakitarajia kuafikiana kuhusu mkataba mpya wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35. (Mail)
Vilabu kadhaa vya juu vya Ligi ya Premia vimearifiwa kuhusu uwezekano wa kupatikana kwa mshambuliaji wa Paris St-Germain wa Brazil Neymar, 31. (90min).
Liverpool, Manchester City na Manchester United wanafuatilia hali ya kandarasi ya kiungo wa kati wa Uingereza Mason Mount mwenye umri wa miaka 24 katika klabu ya Chelsea. (ESPN)
Mshirika nchini Saudi Arabia yameingia kwenye kinyang'anyiro cha kununua Manchester United. (Telegraph - usajili unahitajika)
Wawekezaji wa Qatar wanatayarisha ofa ya ufunguzi yenye thamani ya takriban pauni 5bn kwa United. (Bloomberg)
Bayern Munich wameiambia Manchester United kwamba watahitaji kulipa pauni milioni 18 kumnunua kiungo wa kati wa Austria Marcel Sabitzer, 28, kwa mkataba wa kudumu. (Bild, via Mail)
Real Madrid wanatazamia kumnunua beki wa Manchester United na Ureno Diogo Dalot, 23, ambaye bado hajaongeza mkataba wake Old Trafford. (AS kwa Kihispania)
Arsenal wametuma wasaka vipaji wao kumfuatilia mshambuliaji wa kimataifa wa vijana wa Athletico Paranaense na timu ya taifa ya Brazil Vitor Roque. Barcelona pia wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 ambaye huenda akavutia ada ya zaidi ya pauni milioni 50. (CaughtOffside)
Klabu za Newcastle, Real Madrid, Manchester City na PSG zinavutiwa na winga wa Napoli na Georgia Khvicha Kvaratskhelia, lakini klabu hiyo ya Serie A inataka zaidi ya pauni milioni 50 kumwachilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (90min)
Mkufunzi wa Real Madrid Carlo Ancelotti anasema hajali iwapo kiungo wa Uhispania Marco Asensio, 27, atasaini mkataba mpya katika klabu hiyo au ataondoka. (Mirror)
Southampton na West Ham zinawasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Nice, Terem Moffi, mwenye umri wa miaka 23. (Football Insider)
Kocha wa zamani wa Tottenham, Harry Redknapp atakuwa tayari kurejea kwenye uongozi iwapo Leeds United itamtaka arejee uwanjani. (Mirror)
BBC