Katika kuhakikisha wanawahamasisha mashabiki wao kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe siku ya Jumapili, uongozi wa Yanga umekuja na mbinu ya kufanya hamasa ya mtaa kwa mtaa
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe anaongoza timu hiyo ya hamasa
Jana walianzia Zakiem Mbagala na leo walikuwa Tegeta jijini Dar es salaam
Katika Mikutano yao Wanazungumza na Mashabiki juu ya umuhimu wa kwenda kuishangilia timu yao katika mchezo dhidi ya TP Mazembe huku wakiwauzia tiketi
Pia Wanawapa mashabiki nafasi ya kuzungumza na viongozi wao waandamizi na wachezaji wao kupitia simu
Kamwe amesema wanafanya jitihada ili kuhakikisha mashabiki wanajitokeza kwa wingi siku ya Jumapili lengo likiwa kujaza uwanja wa Benjamin Mkapa

