Kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Raja Casablanca baadae leo, Rais wa heshima klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' amewaahidi wachezaji donge nono kama watashinda mchezo huo
Jana usiku Mo akiongoza na viongozi waandamizi wa klabu ya Simba, alizungumza na wachezaji akiwataka kuhakikisha wanashinda mchezo huo utakaopigwa saa 1 usiku
Katika mahojiano yake na Simba Media, Mo alisema ana imani kubwa wachezaji watapambana na leo ushindi utapatikana
Mo atakuwepo uwanja wa Mkapa leo kuwaongezea hamasa wachezaji wa Simba katika mchezo ambao wanahitaji ushindi









