Mwamuzi wa siku nyingi katika Ligi Kuu ya Premia Lee Mason hatachezesha tena ligi hiyo baada ya kuondoka kwenye bodi ya waamuzi PGMOL kwa makubaliano ya pande mbili
Kuoncoka kwa mwamuzi huyo mwenye umri wa miaka 51 kunakuja siku chache baada ya makosa yake wakati Arsenal ilipotoka sare ya 1-1 na Brentford.
Mason akiwa refa Msaidizi wa VAR, hakutoa mwongozo wa kuangalia kama Ivan Toney ameotea na kuruhusu bao la kusawazisha alilofunga
"Tungependa kumshukuru Lee kwa huduma yake ya kujitolea kitaaluma na tunamtakia kila la heri kwa siku zijazo," taarifa ya PGMOL ilisema.
Sare dhidi ya Brentford iliathiri Arsenal ikiwa sasa inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya kuchapwa 3-1 na Manchester City katika mchezo uliopita
Kuondoka kwa mwamuzi huyo kutawapunguzia hasira mashabiki wa Arsenal lakini Mason huenda akaendelea kubaki lawamani kama Arsenal itakosa ubingwa kwa tofauti ndogo msimu huu