Simba imeshindwa kutamba mbele ya Raja Casablanca katika uwanja wa Benjamin Mkapa wakikubali kipigo cha mabao 3-0
Raja wamedhihirisha ni timu bora pamoja na kuwa wachezaji wa Simba walitakiwa kufanya zaidi ya kile walichofanya
Kipindi cha pili Simba ilikuwa bora zaidi lakini makosa ya kiulinzi hasa timu ilipopanda kushambulia yalipelekea Raja kumaliza mchezo kwa mabao mawili ya dakika za lala salama
Simba sasa inahitaji kwenda kusaka ushindi ugenini dhidi ya Vipers Fc ili kufufua matumaini ya kusonga mbele

