Majira ya saa 1 usiku Wananchi watakuwa pale uwanja wa Benjamin Mkapa kupepetana na TP Mazembe katika mchezo muhimu wa kundi D, michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Yanga inahitaji kushinda mchezo huo ili kuweka hai matumaini ya kutinga robo fainali
Hii ni mara ya tatu Yanga inacheza makundi ya Shirikisho, haikuwahi kufanikiwa kuvuka hatua ya makundi kwenda robo fainali
Hata hivyo ubora wa kikosi cha Yanga wakati huu unawapa mashabiki matumaini kuwa yawezekana msmu huu wanaweza kuishuhudia timu yao hatua ya robo fainali
Ili kufanikisha hilo, Yanga inapaswa kushinda mechi ngumu kama hii ya leo dhidi ya TP Mazembe
Ni wazi hautakuwa mchezo mwepesi, Mazembe sio timu ya kubeza licha ya wengi kuamini haina ubora waliokuwa nao misimu kadhaa nyuma
Vijana wa kocha Nasreddine Nabi wametoka kupoteza mchezo dhidi ya US Monastir hivyo leo wanahitaji kuwapa raha mashabiki wao kwa kutumia vyema uwanja wa nyumbani